Ezekieli 21:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Nami nitapiga makofi,nitatosheleza ghadhabu yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

18. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

19. “Wewe mtu! Chora njia mbili ambapo utapitia upanga wa mfalme wa Babuloni. Njia zote mbili zianzie katika nchi moja. Mwanzoni mwa kila njia utaweka alama ya kuonesha upande mji uliko.

20. Utachora njia upanga utakapopitia kwenda kuufikilia mji wa Raba wa Waamoni, na njia nyingine inayoelekea mji wenye ngome wa Yerusalemu nchini Yuda.

21. Mfalme wa Babuloni anasimama mwanzoni mwa hizo njia mbili, kwenye njia panda, apate kupiga bao. Anatikisa mishale, anaviuliza shauri vinyago vya miungu yake na kuchunguza maini ya mnyama.

Ezekieli 21