1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2. “Wewe mtu! Je, mti wa mzabibu ni bora kuliko miti mingine msituni?
3. Je, mti wake wafaa kutengenezea kitu chochote? Je, watu huweza kutengeneza kigingi kutoka mti huo ili waweze kutundikia vitu?
4. Huo wafaa tu kuwashia moto. Tena moto unapoteketeza sehemu yake ya mwanzo na ya mwisho na kuikausha sehemu ya katikati, je, hiyo yafaa kwa kitu chochote?