4. Mfalme akauliza, “Kuna ofisa yeyote uani?” Ikawa wakati huo Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa ikulu; alikuwa amekuja kwa mfalme kuomba Mordekai auawe kwenye mti wa kuulia ambao alikuwa amekwisha mtayarishia.
5. Basi, watumishi wakamjibu mfalme, “Hamani yuko uani.” Mfalme akasema, “Mkaribishe ndani.”
6. Hamani alipoingia ndani, mfalme akamwuliza, “Je, nimfanyie nini mtu ambaye ningependa sana kumtunukia heshima?” Hamani akafikiria moyoni mwake: “Ni nani huyo ambaye mfalme angependa kumtunukia sana heshima? Bila shaka ni mimi.”
7. Basi, Hamani akamjibu mfalme, “Mtu huyo ambaye mfalme angependa kumtunukia heshima,
8. yafaa watumishi wa mfalme walete mavazi safi ya kitani aliyovaa mfalme na farasi wake mwenyewe,