1. Usiku huo, mfalme hakupata usingizi. Basi, akaamuru kitabu cha kumbukumbu za matukio ya kila siku kiletwe, nacho kikasomwa mbele yake.
2. Ikaonekana ilivyoandikwa jinsi Mordekai alivyongamua njama ya kumwua mfalme iliyokuwa imefanywa na Bigthana na Tereshi, wawili kati ya matowashi wa mfalme waliokuwa walinzi wa vyumba vya mfalme.
3. Mfalme akauliza, “Je, tumempa Mordekai heshima au tuzo gani kwa jambo hili?” Watumishi wake wakamjibu, “Hujafanya kitu kwa ajili yake.”