2 Wakorintho 10:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Kwa vyovyote hatungethubutu kujiweka au kujilinganisha na wale watu wanaojisifia wenyewe. Watu wenye kujifanya wao kuwa kipimo cha kujipimia, na watu wanaojilinganisha wenyewe kwa wenyewe, ni wapumbavu.

13. Lakini sisi hatutajivuna kupita kiasi; kujivuna huko kutabaki katika kile kipimo cha kazi aliyotukabidhi Mungu, kazi ambayo tunaifanya pia kwenu.

14. Hatukuruka mipaka tuliyowekewa wakati tulipokuja kwenu. Sisi tulikuwa wa kwanza kuja kwenu tukiwaleteeni Habari Njema juu ya Kristo.

15. Basi, hatujivunii kazi waliyofanya wengine zaidi ya kipimo tulichopewa; ila tunatumaini kwamba imani yenu itazidi miongoni mwenu kufuatana na kipimo alichotuwekea Mungu.

2 Wakorintho 10