3. Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.
4. Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
5. Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.
6. Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa tambiko na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7. Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.
8. Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana, Hakimu wa haki, atanipa mimi siku ile, na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.