2 Timotheo 2:3-15 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu.

4. Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida, ili aweze kumpendeza mkuu wa jeshi.

5. Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo.

6. Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno.

7. Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu.

8. Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri,

9. na ambayo kwa sababu yake mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo.

10. Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele.

11. Usemi huu ni wa kweli:“Ikiwa tulikufa pamoja naye,tutaishi pia pamoja naye.

12. Tukiendelea kuvumilia,tutatawala pia pamoja naye.Tukimkana,naye pia atatukana.

13. Tukikosa kuwa waaminifu,yeye hubaki mwaminifu daima,maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”

14. Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.

15. Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.

2 Timotheo 2