1. Kisha Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu juu ya mlima Moria ambapo Mwenyezi-Mungu alimtokea Daudi baba yake, mahali ambapo Daudi alikuwa amepachagua, kwenye kiwanja cha kupuria cha Ornani Myebusi.
2. Mfalme Solomoni alianza ujenzi wa hekalu mnamo mwezi wa pili wa mwaka wa nne wa utawala wake.