2 Mambo Ya Nyakati 26:20-22 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Azaria, kuhani mkuu, na wale makuhani wengine, walimtazama, kisha wakaharakisha kumtoa nje; hata yeye mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa maana Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwadhibu.

21. Basi, mfalme Uzia akawa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Alikaa katika nyumba yake ya pekee kwani hakukubaliwa tena kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Naye Yothamu mtoto wake, akatunza jamaa yake huku akitawala wakazi wa nchi.

22. Matendo mengine yote ya mfalme Uzia kutoka mwanzo mpaka mwisho, yaliandikwa na nabii Isaya mwana wa Amozi.

2 Mambo Ya Nyakati 26