1 Yohane 5:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Twajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja, akatupa elimu ili tumjue Mungu wa kweli; tuishi katika muungano na Mungu wa kweli – katika muungano na Mwanae, Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na huu ndio uhai wa milele.

21. Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu!

1 Yohane 5