19. Msimpinge Roho Mtakatifu;
20. msidharau unabii.
21. Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema,
22. na kuepuka kila aina ya uovu.
23. Mungu mwenyewe anayetupatia amani awatakase nyinyi kabisa kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu – roho, mioyo na miili yenu – mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.