1. Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga.
2. Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa.
3. Lakini anayempenda Mungu, huyo anajulikana naye.
4. Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.