1 Wakorintho 10:2-8 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Wote walibatizwa katika umoja na Mose katika lile wingu na katika ile bahari.

3. Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,

4. wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.

5. Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.

6. Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.

7. Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.”

8. Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000.

1 Wakorintho 10