1 Petro 5:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Msiwatawale kwa mabavu hao waliowekwa chini ya ulinzi wenu, bali muwe mfano kwa hilo kundi.

4. Na wakati Mchungaji Mkuu atakapotokea, nyinyi mtapokea taji ya utukufu isiyofifia.

5. Kadhalika nanyi vijana mnapaswa kujiweka chini ya mamlaka ya wazee. Nyinyi nyote mnapaswa kuwa na unyenyekevu mpate kutumikiana; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwajalia neema wanyenyekevu.”

6. Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mungu, ili awainue wakati ufaao.

7. Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni.

1 Petro 5