1 Mambo Ya Nyakati 7:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Bela alikuwa na wana watano: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa zao, na wanajeshi mashujaa. Walioandikishwa kwa kufuata koo, idadi ya wazawa wao ilikuwa 22,034.

8. Bekeri alikuwa na wana tisa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Eliehonai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Wote hawa ni wazawa wa Bekeri.

9. Waliandikishwa kwa koo kulingana na vizazi vyao kama viongozi wa jamaa zao, na idadi ya wazawa wao ilikuwa 20,200, wote wakiwa mashujaa wa vita.

10. Yediaeli alikuwa na mwana mmoja, jina lake Bilhani. Bilhani alikuwa na wana: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari.

1 Mambo Ya Nyakati 7