1 Mambo Ya Nyakati 7:31-39 Biblia Habari Njema (BHN)

31. Beria alikuwa na wana wawili: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

32. Heberi alikuwa na wana watatu: Yafleti, Shomeri na Hothamu, na binti mmoja jina lake Shua.

33. Yafleti pia alikuwa na wana watatu: Pasaki, Bimhali na Ashvathi.

34. Shemeri, nduguye, alikuwa na wana watatu: Roga, Yehuba na Aramu.

35. Na Helemu, ndugu yake mwingine, alikuwa na wana wanne: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

36. Wana wa Sofa walikuwa Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,

37. Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera.

38. Wana wa Yetheri walikuwa Yefune, Pispa na Ara.

39. Wana wa Ula walikuwa Ara, Hanieli na Risia.

1 Mambo Ya Nyakati 7