1 Mambo Ya Nyakati 4:19-38 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Hodia alimwoa dada yake Nahamu ambaye wazawa wake ndio waanzilishi wa kabila la Garmi, lililoishi katika mji wa Keila, na kabila la Maakathi, lililoishi katika mji wa Eshtemoa.

20. Wana wa Shimoni walikuwa Amnoni, Rina, Ben-hanani na Tiloni. Ishi alikuwa na wana wawili: Zohethi na Ben-zohethi.

21. Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa Eri, mwanzilishi wa mji wa Leka, Laada, mwanzilishi wa mji Maresha; ukoo wa wafuma nguo za kitani waliokuwa wakiishi katika mji wa Beth-ashbea;

22. Yokimu na watu walioishi katika mji wa Kozeba; na Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na wakarejea Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.)

23. Hawa ndio wafinyanzi walioishi katika miji ya Netaimu na Gedera, wakimhudumia mfalme.

24. Simeoni alikuwa na wana watano: Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.

25. Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu; Shalumu alimzaa Mibsamu na Mibsamu akamzaa Mishma.

26. Mishma alimzaa Hamueli, aliyemzaa Zakuri, na Zakuri akamzaa Shimei.

27. Shimei alikuwa na wana kumi na sita na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, na jamii yake pia haikuongezeka kama kabila la Yuda.

28. Miji walimokuwa wakiishi ilikuwa Beer-sheba, Molada, Hasar-shuali,

29. Bilha, Ezemu, Toladi;

30. Bethueli, Horma, Siklagi,

31. Beth-markabothi, Hazar-susimu, Beth-biri na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao mpaka wakati wa utawala wa mfalme Daudi.

32. Pia, waliishi katika miji mingine mitano: Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani,

33. pamoja na vijiji kandokando ya miji hiyo huko Baali. Hayo ndiyo yaliyokuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya nasaba yao.

34. Watu wafuatao walikuwa wakuu wa koo zao: Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia,

35. Yoeli, Yehu (mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.)

36. Eliehonai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,

37. Ziza (mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri na mwana wa Shemaya).

38. Jamaa zao waliendelea kuongezeka kwa wingi sana. Hawa waliotajwa majina ni wakuu katika jamaa zao na koo zao ziliongezeka sana.

1 Mambo Ya Nyakati 4