Baada ya Hesroni kufariki, Kalebu alimwoa Efratha, mjane wa Hesroni, baba yake. Efratha alimzalia Kalebu mwana jina lake Ashuri, aliyekuwa mwanzilishi wa mji wa Tekoa.