1 Mambo Ya Nyakati 10:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Vita vilikuwa vikali sana dhidi ya Shauli. Wapiga mishale walipomwona walimjeruhi.

4. Ndipo Shauli alipomwambia mtu aliyembebea silaha, “Chomoa upanga wako unichome nife, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije wakanidhihaki.” Lakini huyo aliyembebea silaha hakuthubutu; kwa sababu aliogopa sana. Hivyo, Shauli alichukua upanga wake mwenyewe akauangukia.

5. Halafu yule aliyembebea silaha alipoona kuwa Shauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake, akafa.

6. Hivyo ndivyo Shauli alivyokufa, yeye na wanawe watatu, na jamaa yake yote.

1 Mambo Ya Nyakati 10