31. Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32. Abrahamu alikuwa na suria aliyeitwa Ketura. Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
33. Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.
34. Isaka, mwana wa Abrahamu, alikuwa na wana wawili: Esau na Israeli.
35. Wana wa Esau walikuwa Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.