25. Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu;
26. Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera,
27. na Tera akamzaa Abramu, ambaye ndiye Abrahamu.
28. Abrahamu alikuwa na watoto wawili wa kiume: Isaka na Ishmaeli.
29. Hivi ndivyo vizazi vyao: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa Nebayothi na wengine ni Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
30. Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
31. Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.